Wateja Vodacom kusajiliwa kielektroniki

Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania inawawezesha wateja wake kufanya usajili wa nambari zao za simu kwa njia ya kielektronikia kupitia simu za mkononi, mfumo ambao unatoa urahisi kwa kila mteja kukamilisha zoezi la usajili ndani ya muda mfupi zaidi wa chini ya saa moja
Kusajili kwa kutumia njia za kawaida, zoezi la usajili huweza kutumia hadi siku kumi na tano kutoka siku mteja alipojaza fomu ili kutoa nafasi kwa wakala aliyesajili kutuma fomu jijini Dar es salaam kwa uhakiki na uthibitisho wa taarifa za msajiliwa.


Mfumo huo wa kielektroniki, mchakato wote wa usajili hukamilishwa kwa njia ya simu ya mkononi kwa kuwa humpa uwezo wakala wa Vodacom kupiga picha kitambulisho cha mteja, kuhakikia taarifa zake na hivyo kuzituma moja kwa moja tayari kwa hatua ya mwisho ya usajili. Kw akutumia TILL maalum
Mfumo huo mpya wa usajili wa kielektroniki unakuja wakati ambapo wateja wetu wamekuwa wakitoa ushirikiano katika utekelezaji wa matakwa ya sheria ya huduma za Kielektroniki za Posta na Mawasiliano - EPOCA inayowataka watumiaji wa simu za mkononi nchini kutotumia laini ya simu isiyosajiliwa.


Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Vodacom Brigita Stephen amesema "Tumekuwa na mafanikio makubwa katika usajili wa nambari za wateja wetu, tunawashukuru sana kwa ushirikiano wanaotupatia katika kutimiza matakwa ya kisheria."
Brigita aliongeza kwa kusema "Mfumo huu wa kielektroniki ni katika juhudi za kuwa na njia mbalimbali kuwawezesha wateja wetu kutojisikia shida katika kusajili nambari zao (SIM),hii ni matokeo ya nia ya wakati wote ya Vodacom kuhakikisha inaendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria, taratibu na kununi zinazosimamia sekta ya mawasiliano na nchi kwa ujumla.
Amesema SIM zote za Vodacom zinazouzwa sokoni huwa haziwezi kuwa hewani kwa matumizi yoyote hadi pale mteja anapokamilisha zoezi la usajili ikiwemo wa awali wakati usajili kamili unapofanyiwa kazi na kinyume cha hapo Vodacom huifungia SIM husika.
Vodacom inaendelea kuwakumbusha mawakala wake wa mauzo ya SIM kuendelea kuwakumbusha wateja umuhimu wa kusajili nambari zao sio tu kwa usalama wao bali pia kuweza kutambulika na kupata msaada kutoka Vodacom pale wanapopatwa na tatizo ikiwemo kwenye huduma za M-pesa, kupoteza simu n.k
Mwaka jana wakati wa zoezi la utekelezaji mpango wa usajili wa nambari za simu chini ya maelekezo ya Mamalaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Vodacom ilizifungia SIM zaidi ya laki nne baada ya kutokuwa zimesajiliwa mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha mpito.
Chini ya Sheria ya EPOCA mteja anaetumia laini ya simu ya mkononi isiyosajiliwa kisheria hutiwa hatiani na hupaswa kulipa faini ya Shilingi 300,000 au na kifungo cha muda usiopoungua miezi sita gerezani au vyote kwa pamoja.