Posted by MOBILE KWETU
Posted on 5:37 AM
Vodacom yaanza majaribio matumizi ya Teknolojia ya LTE ,Wateja maeneo ya Msasani kuanza kunufaika:
Wateja
wa Vodacom sasa wanauwezo wa kutumia teknolojia ya Long Term Evolution -
LTE ambayo ni ya kisasa zaidi ulimwenguni katika utoaji wa huduma za
Mawasiliano na hivyo kupunguza gharama katika kuwasiliana kufuatia
kampuni hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Nokia Siemens kuwawezesha
wateja wake kufanya hivyo katika mradi wa majaribio unaohusisha eneo la
Msasani jijini Dar es salaam.
Pichani Mkuu wa Mawasiliano
wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa
matumizi ya teknolojia ya Long Term Evolution - LTE leo jijini Dar es
salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza na
kushoto ni Mtaalamu kutoka Nokia Siemen Surender Surana. Vodacom
imezindua matumizi ya LTE kwa majaribio katika eneo la Msasani jijini
Dar es salaam.