Home » , , , » Kliniki ya soka ya Man U kufanyika Dar es salaam

Kliniki ya soka ya Man U kufanyika Dar es salaam

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza kufanyika kwa kliniki ya soka ya Kimataifa ya Manchester United hapa Dar es Salaam kuanzania 23 -27 Aprili mwaka huu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea na waandishi wa Habari wakati wa kutangaza Kliniki ya Kimataifa ya mpira wa soka ya Manchester United ambayo itafanyika Jijini Dar es Salaam April 23-27 chini ya wakufunzi kutoka Klabu ya Manchester United. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mashindano ya Vijana Ayoub Nyenzi.
 
Kliniki hiyo ambayo itafanyika kwenye uwanja wa Azama FC (Chamazi Complex Stadium), ina nia ya kuwaendeleza vijana waliofanya vizuri kwenye michuano ya mwaka jana ya kimataifa ambayo ilifanyika Lagos, Nigeria na kushirikisha nchi 12 ambapo timu ya Tanzania ya wasichana iliibuka mabingwa.
Hii ni mara ya pili kwa kliniki kama hiyo kufanyika hapa nchini kufuatia kliniki kama hii liyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa 2011. Kliniki nyingine ilifanyika Nairobi 2012 na Tanzania iliwakilishwa na wavulana watatu na wasichana watatu.
Kama ilivyokuwa kwenye kliniki zilizopita, kliniki ya mwaka huu itaendeshwa na makocha kutoka shule za soka za Klabu ya Manchester United na wanatarajiwa kutoa mafunzo ya awali ya mpira wa miguu kama vile kupiga pasi, kukimbia na mpira, kupiga mashoot, nidhamu na nyingine nyingi.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kliniki hiyo ni sehemu ya mpango kapambe wa Airtel kusaka na kuendeleza vipaji vya soka hapa Tanzania na Barani Afrika kwa ujumla.

LANGUAGE OPTION

POPULAR POSTS

LIVE ON TWITTER

MOBILE INNOVATION

 
Support : Twitter | Facebook | Mail
Copyright © 2014. MOBILE KWETU - All Rights Reserved
Designed by Mobilekwetu. | Powered by Mobilekwetu